22/10/2013

Mungu na Uovu


Swali 

Uovu umetoka wapi? Mungu mwema hawezi kuumba uovu. Basi, uovu umetoka wapi?

Msimamo

Mungu hakuumba uovu, ila
uwezekano wa uovu. Viumbe
vilichagua kutekeleza
uwezekano huo, na uovu
ukatokea.

Hoja

  1. Mungu ni mkamilifu na aliumba viumbe vikamilifu tu.
  2. Mungu aliwazawadia viumbe vyake uhuru wa kutii au kuasi.
  3. Viumbe wakachagua kuasi na kusababisha uovu.
  4. Mungu achukua hatua kuteketeza uovu pasipo kuharibu uhuru wa uchaguzi.

Maelezo Zaidi?

Pata maelekezo kamili ya hoja zinazotetea msimamo wa kibiblia kuhusiana na mada hii. Bonyeza hapa  Majibu ya Wazi kwa Maswali Magum: Mungu na Uovu.pdf Unaweza kushiriki na mwingine kwa kumuelekeza hapa au kuchapa (print) na kumgawia umpendaye kitini hiki. Karibu tena na Mungu akubariki